Hadithi Kuhusu Maisha , Mapenzi , na Jamii

Sunday, August 27, 2006

MARAFIKI WA MTANDAO

Leo nilienda kwa rafiki yangu mmoja hivi kufika kule nikawa natazama TV EA TV , mada ilikuwa inahusu urafiki wa internet waliuliza JE URAFIKI WA MTANDAO NI WA KWELI AU UWONGO ? na kama ni WA KWELI , HUWA UNADUMU NA KUENDELEA DAIMA NA MILELE ?

Hili ni swali zuri sana na linavutia sana kwa upande mmoja au mwingine , pale nilienda kufanya shuguliz ingine na maongezi kidogo sikuweza kuchangia chochote zaidi ya kusikiliza mawazo ya watu wengi , wengi waliochangia sio werevu wanafikiri katika internet haswa chatrooms ni sehemu za maasi siku zote na sehemu mbaya .

Nachangia kama ifutavyo

Mimi nimekuwa natumia internet kwa karibia miaka 10 sasa , mwanzo nilianza kuitumia nikiwa nchini Kenya nikiwa shule ya msingi nakumbuka mwaka 1996 hivi sijui nilikuwa darasa la 5 hivi sina hakika sana , hapa nilikuwa natumia internet lakini kwa ajili ya kucheza game and so on

Niliporudi nyumbani kwa likizo baba yetu alitufungia internet nyumbani tukawa tunaitumia internet kwa mambo mengi hapo nilijifunza mengi na kuelewa mengi haswa swala hili kuu la mahusiano katika internet .

Lakini sikutafuta marafiki wala mahusiano katika internet mpaka mwaka 2000 nilimaliza masomo ya secondary kwa sababu nilikuwa niko huru zaidi na maisha yangu na kadhalika mwaka 2001 nilianza chuo , hapo maisha yangu yalibadilika na kuanza kuwa na mahusiano kadha wa kadha katika internet .

Mwaka 2000 niliijua www.kenyaniyetu.com mwaka uliofatia niliijua www.darhotwire.com na site zingine lukuki nikaanza kuchat humu , rafiki yangu wa kwanza kabisa ambaye nilielewana nae na ambaye mpaka sasa hivi ni rafiki yangu anaitwa Happy , siku hizi anaitwa Kiki jina lake halisi ni Anneke , huyu naweza kusema ananijua sana kwasababu nilimkuta kipindi hicho yeye ndio anaanza kutumia computer hajui nikamfundisha na kuelewana nae sana .

Mpaka leo mwaka 2006 bado niko www.darhotwire.com niko katika site zingine chache ambazo nazo ni nzuri ila zote hizo hazina members wengi na sio rahisi kuendelea kutokana na matatizo kadhaa kwanza ubabe na nyingi haziko huru , zinaegemea upande Fulani mfano ukienda www.jambotanzania.net hii ni site mashabiki wengi wa humu wako CCM maana yake ukiongea vitu vingine ambayo ni tofauti na CCM basi wanakuchukia na kuonekana adui wa wengi , au ukiongea vitu ambayo wengi hawapendi kwasababu wengi hawako huru wanakuona hufai muasi .

Turudi katika darhotwire , kwa kweli nimehudhuria harusi zaidi ya 8 za wanachama wa darhotwire ambao walikuwa wanachat na mimi na wakaowana na nib ado rafiki zangu kasoro moja tu ndio imevunjika kwa sababu kadhaa lakini hawachukiani bado wanakuja chat na kuongea ingawa hawaishi pamoja mpaka leo hii .

Na kwa bahati nzuri , mwezi wa 9 mwaka huu kuna harusi ingine ntaenda ya member wa DHW inafanyikia mkoani arusha , mwezi wa 12 pia kuna harusi ingine inafanyikia hapa hapa dare s salaam na mwezi wa 3 mwaka kesho ni harusi lakini hii inafanyikia nchini oman nayo ni members wa dhw .

Naomba nikujulishe kwamba , siku zote ukiwa katika internet ukitaka marafiki au urafiki uwe muwazi , maana yake , kwanza kaa ona watu wanaongea nini na wewe ongea uwe muwazo na elezea kile unachojisikia na kufikiria hakuna atakayekucheka kama anakucheka basi kaa pembeni usibishane nae kesho yake njoo rudi tena ongea huko ndio kujifunza kisha mwisho wa siku utajua kila mtu anafikiria nini yaani unaweza kuhandle watu .

Ntakupa mfano mmoja niliingia www.jambotanzania.net , hapa niliona watu wengi , basi sikupenda kuwajua kwa kuchat na kila mtu , nilitaka kuwajua kwa kuwachokoza na kuwatania , hapa nilijua chat hii haina marafiki wa kweli , wengi ni marafiki wa ngono , wababaishaji , yaani mtu hawataki kuwa wawazi na kuelezana ukweli .

Ukishamwona rafiki ni muongo au unamuuliza swali anasita sita , ukimuuliza mwenzake anakujibu tofauti ogopa sana , wengine wanakuwa na mission zao katika hizo chat na maisha ya kawaida kwahiyo chunga sana usiingie gizani na ukashindwa kutoka na mambo ya kuangalia na kujifunza .

Jua kwamba watu wanatumia chatrooms kama vijiwe vya kupumzikia , unajua mtu akikaa kijiweni hana kazi anavuta bangi sigara na kutumia madawa ya kulevya akiona msichana anapita ataenda kuongea nae kumtaka afanye nae ngono tu halafu amuache ?? haya mambo yako kwahiyo mtu yuko radhi anashinda siku nzima apata mwanaume au mwanamke wa saizi yake au mdogo wake ahalalishe mambo yake .

Wengine ndio hivyo , Malaya wanajiuza kutumia internet , katika www.jambotanzania.net siku moja niliingilia mazungumzo ya jamaa mmoja analalamika kwamba amepata msichana katika jambo Tanzania lakini huyo msichana alikuwa anacheza ( strip ) katika webcam kwa raifki yake mwingine amuone halafu aende kwake mambo kama hayo .

Mwingine niliongea nae alikuwa anatafuta wasichana ili awapeleke katika danguro huko ulaya , niliongea nae sana siku hiyo kupitia chatroom ya jambotanzania , ni mtu ambaye wameshamweka operator , huyu jamaa alikuwa anamtaka dada mmoja anaitwa TASHNA lakini sikupenda kumwambia TASHNA kuhusu hili nilinyamaza tu mpaka sasa nimenyamaza .

Pamoja na hizo ndoa zinazofungwa , ni mara chache kukuta marafiki wa kweli na wenye nia nzuri na wewe , wengi wao kama hivyo nilivyokuambia ni waongo , matapeli , wafanya biashara haramu za kuuza watu , wengine majambazi wa kutumia mtandao na mambo kama hayo ila utamwona anaongea na wewe lakini ukianza kumdadisi anakimbia hataki umjue au anakuunganisha na watu wengine au anakutusi mambo kama hayo .

USHAURI WA BURE : mara nyingi mtu akikutania sana au akiwa anapenda kukutania na kukuongelesha sio kwamba anakuchukia wengi ni wale wanaopenda kukujua wewe zaidi , umeshaona mtu hutaki kuongea nae lakini anaulizia marafiki zako kama wewe mzima unaendeleaje na maisha yako ?? huyu ni rafiki mzuri anapenda kukujua na kuongea na wewe mambo mengi , mtu kama huyu ukishirikiana nae unaweza kupata faida nyingi na kujuana na watu wengi zaidi maishani wenye staha kama yeye na silka .

Utani wa katika internet haswa wa main chat , usiupe uzito sana , lakini akija prv yako na kuanza kukutusi au akienda chemba kwa rafiki yako na kuanza kukusema wewe na kukutusi huyo ndio unapaswa umnyooshee kidole lakini usijali sana jifanye hujui , uwe mtulivu mfuatilie umjue vizuri malengo yake ni nini .

Kuna wengine walevi pale wako majumbani wanapumzika lakini anaingia chat na kuanza kutusi watu , huyu ana matatizo yake , wengine wamegombana na wapenzi wao wanakuja katika chat kupooza maugomvi yao , wengine yamewakuta mambo mengi anakuja chat kupunguza makali .

MFANO : kuna dada anaitwa Kiki au Happy huyu dada , ukimuuliza kuhusu maisha yake ya kimapenzi au habari za mpenzi wake hapendi kabisa kwasababu alikutana na mwanaume mmoja mswahili kama mimi akamdanganya mpaka leo dada hana hamu na mwafrika kwahiyo yeye anajua marafiki wa mtandao walivyo , ukimtania kuhusu mapenzi huwa anatoka katika chat kinamuuma unamkumbusha machungu ya mpenzi wake yule muongo .

Makosa ni yake kwasababu wakati wanajuwana , Happy hakuwa anaelewana na mimi , huyu mvulana alikuwa anajua Kiswahili akawa ananiambia “ WE UNAMTETEA HUYO MANZI ?? “ sasa atakiona na ni kweli wakaenda sawa kiki akaingia mkenge akapatikana ametumia hela kibao kumtumia yule mswahili Kenya mpaka basi mwishowe akaja kujuta kumbe alikuwa anatupa ??


UTAJENGAJE URAFIKI MZURI KATIKA INTERNET

Labda kwanza nikupe hints za rafiki mzuri wa internet .

Unajua jina lake na taarifa zake kabla ya kuanzia kuzungumza kahusu mambo mengine .
Mnashabihiana kwa vitu viwili au zaidi katika maisha yenu ya kila siku
Ni mkweli
Ni mshauri mzuri
Anayekubali ukweli ( kama rafiki amekosea mwambie ukweli ili ajifunze kama unaogopa kumwambia ukweli kwasababu tu urafiki utakufa au kuchukiwa basin a wewe sio rafiki wa kweli hufai kuwa rafiki , mimi siogopi kumwambia mtu kitu kinachonigusa moyoni hawa mbele za watu na siogopi utafiki kuisha kama unavyoona hapo kila siku ninapata marafiki na tunatembeleana bora nipoteze urafiki na wewe wengine wabaki ambao wanapenda ukweli .
Mvumilivu ( hii maana yake akitaniwa hata kama ni utani wa kweli atakuuliza kwanini umemwambia vile utamweleza kama unamtania anakimbia anakasirika huyo sio rafiki mzuri siku takuumiza wewe )
Muwazi ( kwa kuwa munaaminiana atakuambia mambo mengi kuhusu yeye umjue vizuri na kama unakasoro atakurekebisha )
Hata makundi ( haya makundi wasichana ndio wanayo zaidi , unakuta mnachat watu zaidi ya 50 lakini kuna kikundi kimoja cha wasichana 10 hivi ambao wanajifanya wao ndio wao usipende kujiunga katika vikundi kama hivi )
Mbadilikaji ( hii maana yake kila ukikutana nae au kuongea nae atakuja na mambo mapya ambayo yatafanya urafiki wenu udumu zaidi , mfano atakuambia kuhusu weekend yake , labda kama alienda disco jinsi ilivyokuwa )
Sio mpenda ngono ( mwingine atakuja kuanza kuongelea ngono muda wote saa yoyote ile , huyu pia sio rafiki mzuri , anaweza kuongelea ngono kama ameulizwa ila kama rafiki hutakiwi kuongelea ngono haswa kama unayeongea nae hamhusiani kingono )
Mwanaharakati ( kila mtu ni mwanaharakati lakini yeye anatakiwa awe mwanaharakati wa kitu Fulani katika fani yake , utakua unajua ninarafiki anajua mambo haya kwake utapata msaada Fulani au chochote kipya )
Sio tegemezi ( mambo ya utegemezi nahisi unajua , kwetu Tanzania mtu akishakuwa rafiki yako haswa msichana ndio njia ya kuanza kukuomba vocha za simu hata kama hajui hali yako halafu anawasiliana mashoga zake story za ajabu ajabu tu )

JINSI YA KUHEPA MARAFIKI WAONGO

a) Kama ndio unaanza kuongea nae leo mpe kama miezi 3 hivi kabla hujamwambia ukweli kuhusu wewe .
b) Kama wewe ni mwanaume ( ukipewa namba usipige hapo hapo , mpigie siku 3 hivi baada ya kukupa namba ) ukifanya hivi utajua kama rafiki yako ni makini au lah wengi wanapoteza namba ukipiga atakuuliza wewe ni nani mambo kama hayo hata kama alikupigia na mliongea .
c) Usimwambie mtu historia yako kamili haswa ile muhimu
d) Jua kwamba chat au internet ni mtandao wa watu wengi , ukiwa katika chatrooms usipende uwongo bora usiseme kabisa ukimdanganya shy ukija kumwambia ukweli mentor huwezi jua kama shy na menta ni marafiki wataambiana kisha wewe ndio unakuwa mbaya mwisho wa siku .
e) Usipende kwenda chemba , hizi wengi huzitumia kwa majaribio
f) Kama kuna mazungumzo yoyote muhimu usipende kutumia simu au emails , bora ukutane na mtu huyo kama kweli ana mazungumzo ya kweli na wewe na jinsi ya kukutana soma point ya a
g) Jua kwamba wengi haswa wanaume wako katika chat kutafuta wasichana wa kuwamalizia haja zao za kimapenzi , usikubalia kudanganywa kwa fedha kama anafedha nyingi ujue hauko mwenyewe kuna wengine katika list mbaya zaidi hata kama ataahidi kutumia kondom usikubali utajua mwenyewe madhara ya kondom kwa binadamu kwanza kondom nyingi siko sokoni kwa majaribio .
h) Usipende kuridhika na maneno tu , uwe mbunifu wa kumuuliza mtu maswali ya kurudia mara kwa mara , kama umri wake , jina lake , namba ya simu vitu kama hivyo ili ujue kama kweli ni muwazi .
i) Usiulize taarifa za mtu mwingine kwa mwenzako tafuta mwenyewe , wengi wanapenda kutumia majina tofauti unaweza kuuliza taarifa kwa mwingine kumbe ni huyo huyo amebadili jina tu au ni rafiki yake wa karibu lakini hujui .
j) Mwisho wa yote , panda kuchangia mada ambazo watu huongelea katika forums au chat , kama unashinda usikae kimya tafuta cha kufanya kuliko kwenda chemba za watu , huko ndiyo yatakukuta au cha kufanya usiingie chat soma magazeti na mambo mengine muhimu .
k) Jua katika chat watu wanakuja kwa maana tofauti , wengine ndio hivyo wameadhirika wanausambaza kama jamaa mmoja wa CELTEL huyu anajulikana anaingia chatroom nyingi hudanganya wasichana kwa fedha tu wanakubali kwenda nae , wengi huvitumia vijiwe kuchukua watu haswa wasichana wakafanye biashara za ukahaba nje ya nchi bila ya wao kuwa na ufahamu huo .
l) Mimi nafuatilia maisha ya watu katika internet ili kuokoa baadhi ya marafiki zangu ambao ni wakaribu sana katika mambo mengi sipendi kuwaona wanaangamia au kufanyiwa vitu vya ajabu ajabu na kama wewe umesoma mpaka hapa ni rafiki yangu pia tena ndugu yangu wa karibu .

UKIMWI UNATESA

Juzi nilipoangalia gazeti la Alasiri ukurasa wa 2 niliona picha ya kijana mmoja raia wa Haiti , Kijana huyo yuko nchini Canada katika Mkutano Mkuu wa Ukimwi duniani , kijana huyu amevaa nguo nadhifu anapendeza pembeni yake anapicha inayomwonyesha wakati alipokuwa na virusi vya ukimwi kabla hajaanza kutumia ARV dawa za kupunguza makali ya ukimwi .

Leo katika the guardian nimeona picha hiyo hiyo , lakini ikiwa kubwa zaidi , niliangalia sana nikafikiria mhariri wa gazeti anapoamua kuruhusu picha kama hizi ziwekwe kwenye magazeti ana maanisha nini kwa vijana wenzake wanaoangalia , haswa wa kwetu huku afrika sana Tanzania ambako na mimi mwenyewe nipo .

Ninapoona picha kama zile na kufikiria ugonjwa wa ukimwi napata utata , wanavyoamua kutuonyesha picha kama zile maana yake kijana sasa una ruhusa ya kufanya ngono unavyotaka ukiupata si kuna dawa za kupunguza makali ya ukimwi tena serikali inatoa bure si uhondo huo ??

Siku moja nilienda duka la kuuza dawa za binadamu karibu na nyimbani sasa nikawa nashika zile aina za kondom , nikashika zile za bei ya juu yaani alfu 2000 zinauzwa , nikashika mpaka hizi za bei rahisi na bure , nikajiuliza kwanini kondom zinabei tofauti wakati zote kazi yake ni moja kuzuia magonjwa na mambo mengine ?

Nikamuuliza huyu jamaa kuhusu hili jambo akaniambia kwamba zile kondom za raha zimeletwa kwa majaribio na serikali ya nchi Fulani hapa Tanzania , kwahiyo wao yaani wauza hizo kondom ndio watapeleka kwa serikali data kuhusu matumizi yake , na ni kweli sasa hivi raha kondom zinapungua , kuna dume kondoms zote toka ubalizi wa Marekani .

Halafu nafikiria na kujihisi baridi kabisa nikisoma sehemu kadhaa kuhusu ugonjwa wa ukimwi unavyosambaa kwa kasi kubwa hapa Tanzania kutokana na takwimu za mwaka huu mwezi wa 6 , katika vijana 10 basi 2.5 wameadhirika na ukimwi na wengine 3 wanafuatia au wakati mwingine unaweza kukuta wenyewe hawajijui kama wameadhirika au la .

Hawajijui kwasababu huu ugonjwa umefanywa kama vile jangwa kubwa sana , yaani kijana umwambie kupima ukimwi ??? bora musiwe marafiki kuliko kupima manake kupima wengi wanajihisi ameshaambukizwa ukimwi tayari kwahiyo kwenda kupima anaona ni ngumu zaidi , kwa kifupi hawajiamini .

Wengi katika uhusiano wao au mahusiano wanapenda kupima ukimwi siku za mwanzo tu , yaani amejuwana na mtu mwezi wa 1 mwezi wa 2 wanaenda kupima siku hiyo hiyo akipata majibu yake basi wanaanza tendo la ndoa , huu nao ni mtego wengine , vijana hapa sio wavumilivu .

Saaa zingine kijana anadanganywa na wenzake kwamba usipofanya tendo la ndoa unaonekana sio kijana kamili mwanaume yaani , hapa kijana kama hana mwanamke wa kuokota anaamua kwenda sehemu kama bar hivi , au katika madanguro na kutafuta msichana wa kujipooza kwa hisia hizo .

Mwisho wa yote ni jamii nzima ya kiafrika imejijengea mila na desturi za kupenda ngono , kupita kiasi na isiyo na mipaka , mfano mimi nilishawi kwend anyumbani kwetu mara kwa mara , baba yangu akaniuliza kwanini sina rafiki wa kimapenzi ?? Kwanini sitembei na wasichana maswali kama hayo , kwa kijana mwingine hii ni green light kwamba atafute msichana awe nae ili aonekane na wazazi wake au jamii husika kwamba yeye ni mwanaume na ananguvu za kiume vitu kama hivyo .

Ni wakati sasa wa kila mtu haswa vijana ajitambue kwamba yeye anauwezo wa kubadilisha maisha yake na kuyafanya sio ya waathirika wa ugonjwa wa ukimwi na magonjwa mengine ya zinaaa , ngono sio lazima kwa maisha ya binadamu , na kwanza utafanyaje ngono wakati hujahalalishwa ? utafanye ngono kujifurahisha au kama mazoezi ? kuna mambo mengi ya kufanya na mazuri yanavutia .

Kila mtu na nafasi yake aliyonayo anaweza kubadilisha maisha yake na kufuata njia iliyonyooka , sio lazima uokoke au uwe muumini mzuri wa dini , katika dini wanakataza baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuepusha na janga la ukimwi na mimba zisizo na mpango .

Wewe una nafasi kwa uwezo ulio nao kuujua ukweli kuhusu ukimwi , Serikali imetumia hela nyingi sana mpaka hapo ulipofikia kukufanya uwe hivyo ulivyo sasa hivi , halafu unataka kitendo cha dakika chache ndio kikufanye uonekane wewe si mali kitu yaani utie hasara kwa familia yako , serikali na taifa nzima ?

USIKU WA GIZA

Wewe usiku wako labda unautumia kwa ajili ya kulala tu usiku unakaa unaota ndoto nzuri wakati mwingine za kutisha na kuchekesha ndoto hizo wakati mwingine ni kama zinakuhabarisha mambo unayokuja kukutana nayo siku za mbeleni kama prophecy wengine husema , ndio wewe unaona na kushangilia usiku wako , wengine usiku huu huutumia kwa kazi zao mfano polisi na walinzi wao hutumia saa za usiku kulinda watu wao na taifa kwa ujumla , wengine kama Malaya huutumia usiku huu kwa kujiuza na kufanya biashara za miili yao , wengine kazi yao ni kucheza muziki kwahiyo saa za usiku kwao ni kucheza muziki kuburudisha wengine na wengine ni majambazi usiku wa giza wao huutumia kurubuni watu , kuuwa watu ili wajipatie chochote kile kwa maisha yao ya kila siku , wengine wa wanga na wachawi hutumia usiku kama wakati wao wa kufanya mambo yao ya kishirikina bila kuonekana na roho za kawaida kwahiyo kila mtu ana mambo yake wakati wa usiku .

Basi bwana nyumbani kwetu tulikuwa na ngombe kama 3 hivi huko moshi vijijini , hawa ngombe wote ni wakike , walivyokuwa wakubwa babu yetu akaamua kuwapeleka kwa dume awapande ili waweze kuzaa watoto na tupate ndama , maziwa na maziwa mengine yawe ni ya kuuza kwa watu wengine katika mtaa huo huko vijijini .

Haya ngombe walipandwa , mmoja akazaa lakini ndama wake akafa huyu mwingine ndama wake hakufa lakini yule ndama alikufa katika mazingira ya kutatanisha daktari wa kujiji alivyokuja kuangalia hakukuta alama yoyote ya sumu au kama amekula chakula chochote kile kibaya basi tukamwachia mola.

Ngombe bwana wakawa wanatoa lita 20 mpaka 30 kwa siku moja babu yetu alifurahi sana , lakini baada ya wiki 2 hivi hali ikaanza kuwa tofauti sana , yaani yule ngombe hatowi maziwa yanakuwa kama vile yamekamuliwa usiku kutwa .

Siku moja tumakaa kibarazani babu yetu akawa anatupa hadithi za hapa na pale jirani yetu akaja alipofika pale akamwambia babu kuhusu yule mzee wa mtaa wa pili anavyokuja kuiba maziwa usiku kwa njia za kishirikina akamweleza kila kitu .

Lakini babu hakuwa na nguvu zozote basi bwana ikabidi yule mzee atupe dawa mimi na kaka yangu mmoja ili yule mzee akija usiku tuweze kumkamata na kumwadhibu usiku unaofuatia akatuelekeza cha kufanya kila kitu .

Usiku ukafika , tukajipaka zile dawa tukakaa sehemu karibu na banda la ngombe tukasikia kengele zinalia kutokea mbali ngrii ngrii ngrii , tukakaa kimya , ndio tukaona mzee mmoja anakuja miguu yake ikiwa juu na mikono chini yaani anatembea kwa mikono badala ya kutembea kwa miguu huku akiruka ruka na kuimba nyimbo zake .

Yule mzee akufika pale ngombe alipo akatowa ndoo yake nyuma ya mgongo wakati anakuja hakuwa na ndoo wala hakubeba chochote hiyo ndoo ilikuwa hewani tu , akaitowa pale akaweka akaanza kuchukuwa maziwa toka kwa ngombe haraka haraka akavamia ngombe wa pili , basi kabla hajafika mbali sisi tukafika pale nyuma yake na kumkamata .

Mimi nilimkamata , lakini kaka yangu alikuwa na hasira sana , ndio yeye akaanz akumpiga kichwani mzee wa watu akaanza kuomba msamaha akasema hatorudia tena , basi tulioijisahau tu , fyuuu yule mzee aligeuka moto , kaka yangu alishituka ameshika moto lakini alikuwa ameshajisahau ule moto ulimchoma karibu mwili mzima .

Kaka yangu alimwachia moto ukaendelea kuwaka tu mimi nikakimbilia ndani lakini ghafla moto ule ukaisha kimaajabu , nikatoka tena nje nikakuta kaka yangu ameungua sana hajiwezi , nikasikia sauti kali inaniambia na mukome mimi sio saizi yenu halafu mvua ya mawe ikaanza kunyesha .

Nilikimbia sikuweza kumsaidia kaka yangu kwa sababu mawe yalikuwa makubwa yamenidondokea yananiumiza nikamwacha pale kuridi nyumbani kuja kulala , basi kesho yake asubuhi tunaamka , ndio hivyo kaka akawa chizi tuseme kichaa hakuweza tena kuwa na akili timamu .

Sikuamini hali hiyo mpaka leo hii , nikaendelea tu kuishi kwa nguvu za maulana , siku moja tukaamua kumpeleka kaka yetu kwa kakobe akaombewe aweze kupona ugonjwa wake , basi tulipofika pale ubungo tu gari yetu ilipata ajali mbaya lakini wote tulisalimika .

Tulishindwa kumpeleka kaka kwa kakobe , siku ingine ikabidi tumpeleke kwa waganga huko mkoani tanga kwa wataalamu tuone kama watamponya au la , kabla ya kufika kwa yule mganga , tulisikia sauti inatuamrisha kugeuza njia tusielekee kule tunapoenda .

Dereva alipoendeleza mwendo ili tufike basi gari ilikumbana na upepo mkubwa sana ghafla gari ile ilisimama tairi zikapata pancha , dakika 5 baadaye nilipoangalia katika kiti cha dereva nikakuta simba amesimama pale yaani ndio ameshikiria ile usikanio wa gari .

Tulipiga sana kelele , tukaliacha lile gari pale tukapanda basi kuelekea kule tunapotaka kwenda , basi bwana tulivyopita vituo 2 vya mwanzo kondakta akapotea ghafla , kukawa na dereva tu .

Nyuma yetu jamaa mmoja akawa anasema ashushwe , kufika kituo cha 3 dereva akaangalia nyuma nani anataka kushuka hakuona mtu yaaani alikuwa ni mtu hewa , tuligopa sana basi dereva alikimbiza gari tu .

Mwishowe tukafika pale kwa mganga , tukamweleza shida zetu basi tukawa tunalala nyumbani kwake kwa siku kama 4 hivi hizo siku zilikuwa za balaa sana mimi nilikuwa nimempeleka kaka yangu nilikuwa na akili timamu nikajionea mwenyewe mambo yalivyo katika usiku huo wa giza .
Siku ya kwanza wakati niko pale nimelala kitandani usiku wa manane nilishituka ghafla nikamwona babu yangu mzaa babu amekaa kitandani amevaa nguo nyeupe kabisa ananiangalia huku machozi yakimtoka , sikuelewa kwa nini analia vile mimi sikuweza kufungua mdomo kusema chochote .

Siku iliyofuatia basi bwana nikachukuwa zangu ndoano nikaenda kuvua samaki mtoni na vijana wengine wa pale , nikaanza kuvua na kuvua , mpaka jioni kikafikia kigiza kidogo hivi wale jamaa waliniacha mwenyewe .

Kila nikivuta ndoani naona ni nzito sana nikafurahi nimeona samaki mkubwa lakini huyu anatisha zaidi yaani mzito sana sikuamini nikaendelea kuvuta tu ile kamba kuvuta kuvuta mpaka mwisho kuangalia vizuri kumbe nilikuwa namvuta mama yangu mzazi na ndoani toka mtoni .

Kweli alifika pale nikamburuta kwenda kumwangalia ni kweli yeye hana tofauti , kwenda kumuuliza kunani akawa analalamika tu yoo yoona mwanangu unaniuwa , mwanangu unaniuwa hivi hivi , huyooo akakata roho , ghafla tu akadondoka chini na huo ukawa mwisho wake .

Asubuhi naamka napigiwa simu toka nyumbani kuambiwa kwamba mama yangu amefariki dunia nyumbani , kwahiyo niende haraka , nikamwacha kaka yangu kwa mganga mimi nikaelekea zangu nyumbani kwenda kufanya mambo mengine ya msiba .

Msiba ulikuwa mkubwa sana watu wengi wakubwa kwa wadogo , ukafika wakati wa kumzika , kwenda kuliingiza kaburini tukamfukia na kumfunika kabisa wakati watu tunaanza kutoka makaburini ghalfa lile kaburi likafunuka likatoka nyoka kubwa sana mule kaburini .

Watu walianza kulishambulia kwa mapanga na majembe mpaka wakaliuwa pale pale , bado katika mawazo yangu siamini nini kinachoendelea katika maisha yangu , tulimaliza msiba ule , kesho yake jumapili nikaamka kuelekea kanisani .

Wakati napanda mitaani kwenda kanisani nikamwona mama yangu anatembea na mimii pembeni yangu lakini hasemi kitu , nikijaribu kumkimbia yeye ananishika , lakini nikimwangalia sioni kichwa chake ila anaonekana ni yeye kila nikijaribu kugeuka sioni kitu .

Nikawahi kanisani bwana kwenda katika misa ya asubuhi ili nikitoka pale niwahii kuchukuwa gari nirudi zangu tanga kwa ajili ya kumcheki kaka yangu na mambo yake ya kulogwa .

Kweli nikafanikiwa kwenda mpaka tanga , kufika kule nikamwona kaka yangu lakini yule mganga hakwepo basi niaanza kucheki katika vyumba vyake vitu anavyotumia mambo kama hayo .

Nikafika chumba kimoja kuangalia mule ndani nikaona kichwa cha mama yangu , na mikono yake amekatwa katwa kama mbuzi , nikaona pia kichwa cha babu yangu kinavuja damu na kimakatwa na panga moja .

Nikafunga ule mlango nikatoka nje , basi ndio nikashtuka toka usingizini kumbe nilikuwa naota ndoto za ajabu hivi , lakini imenifunza mambo

Woooow

SAFARI YANGU YA MBEYA

Duniani kuna mambo mengi sana , ambayo mengine ni kama vibaya kuhadithia kwa wengine kama labda ni wenyeji wa huko au labda kama wana mahusiano na kitu hicho inakuwa mbaya haswa kwa wale wasiopenda kujua ukweli wa mambo , lakini wote tunakubaliana kitu kimoja bila kusemeana ukweli hakuna mafanikio yanayoweza kufikiwa na binadamu kwa njia yoyote ile hata kwa nini .

Ntakupa mifano michache mfano huku afrika na sehemu zingine za bara asia na amerika ya kusini , viongozi ni waongo , wamewajengea mpaka watoto wao na vizazi vingine uwongo kiasi kwamba mtu akisema ukweli anaonekana muasi mbaguzi au pengine mchonganishi wanabakia kulalia uongo siku zote hawaendelezi vizazi na watoto wao katika secta ya sayansi na elimu ambayo inahitahi ukweli na uwazi kila kitu uwongo na ulaghai

Hata katika mila na desturi , huku afrika mila na desturi za uongo ni fani , angalia hili suala la ushirikina ?? ushirikina ni mali ya mwafrika na huku imejaa sana lakini ushirikina ni uwongo mtupu ni ujanja ambao mwingine akifundishwa ana adapt na unaweza kutumika kwa faida nyingi tu katika maendeleo na makuzi ya watu wengine hii ni sayansi inayohitaji kuwekwa wazi ila ndio hivyo uwongo umetuzidi mpaka tunajichukia .

Mimi huwa napenda kusema kila ninachojisia kinanivutia na nimeshuhudia mwenyewe kwahiyo sio uwongo napenda kuandika kwa njia ya hadithi au makala kwa watu haswa mafariki zangu , juzi nilikuwa mkoani mbeya na hayo niliyoandika ndio hali halisi ya watu wa mkoa ule wanavyoishi wengi wao hata kama wakikataa na kubisha wanakataa lakini wajomba zao , mama zao , wadogo zao na majirani zao wanaangamia .

Haswa katika hili suala tata la ugonjwa wa ukimwi , huu tuuangalie kwa pande 3 kuu yaani mimi , wewe na yule ( wale ) tuna nafasi gani katika kuendeleza jamii zilizobora ambazo hazisumbuliwi na jinamizi la ugonjwa wa ukimwi wala matatizo yoyote wote wakue vizuri waje kuwa taifa bora watoe mchango kwa majirani zao na vizazi vijavyo ?

Usijali bwana ( KILA MTU NA MAISHA YAKE AU SIO )

Ehe vipi mambo hapo ulipo ??


Hapa ni salama sana , maisha ni bam bam naweza kusema , sasa hivi ni mchana wa saa 6 hivi inaelekea saa 7 kamili , ni lunch time kwa wengine ila mimi huwa nakula chakula cha mchana kuanzia saa 9 hivi au saa 10 jioni halafu usiku huwa sili chakula napenda kula samaki na karanga hiyo ndio furaha ya maisha yangu ya kila siku , kila mtu anaamua na kutenda anachoona kinafaa au sio ?

Basi kipindi hichi cha karibuni wiki hizi 2 nilienda mbeya kwa ajili ya kazi katika offisi moja hili ni shirika la uingereza kazi yake ni kusaidia watu wa manispaa na miji katika ukusanyaji wa kodi na mapato na katika kuwafundisha zaidi kuendana na uchumi wa dunia jinsi unavyokuwa kila siku .

Shiriki hili tuna mkataba nalo wa mambo ya ufundi na shuguli zingine zinazohusu data na ukaguzi wa vifaa vyao vya mawasiliano , kutokana na mkataba huu kila baada ya miezi 3 lazima niende mkoani mbeya angalau kwa wiki moja kuangalia hizo mishine zao n akutatua matatizo yao kama yapo na maisha yanaendelea .

Kwahiyo wiki hizi ndio nilienda mimi na walishanizoea , lakini mwaka huu nilijuwana na dada mmoja hivi anafanya kazi pembeni mwa shirika hili yeye ni mama mahesabu , ananipenda sana mimi na wakati mwingine akinipigia simu huwa ananieleza kuhusu ngono jinsi tukikutana atakavyo nikumbatia , mabusu na mahaba mengine mazito mazito yaani amejichambua sana kuhusu maisha yake kule na anavyonizimia mimi .

Huyu dada alipata taarifa kwamba ntaenda kule , lakini huyu dada sijawahi kukutana nae zaidi ya kuchat nae tu na kuongea katika simu , dada wa watu alijiandaa sana kwa ajili ya kunipokea nikalale kwake yaani kitandani kwake na ile baridi anavyonihadithia anapenda kupata joto langu mambo kama hayo .

Nikatoka zangu huku jumatatu asubuhi saa 12 hivi kwa usafari wa Scandinavia , nilikatiwa tiketi mpaka mbeya lakini nilivyofika iringa pale makambako nilishuka katika gari hilo nikapanda basi lingine nilijua tu huyu dada atakuwa ameshaambiwa naenda na basi gani wakanipokee stendi ya mabasi hapo nilishmkwepa kwa kiasi kikubwa .

Muda wa saa 1 hivi usiku basi lilikuwa limeshaingia mbeya mjini mimi sikwenda kule mwanjelwa nikashukia sehemu moja inaitwa fire , hapo pembeni yake wala sikuchukuwa hoteli , nilipeleka vitu vyangu katika nyumba ndogo za wageni kwanza nione hali ya mambo inavyoenda kabla sijaamua mambo mengine .

Saa 3 hivi usiku ikatimia kama nilivyootea yule dada akanipigia kuniuliza kama nimeshafika mbeya , nilimuuliza amejuaje kama naenda mbeya ? akasema ameambiwa na receptionist wa pale kwa mkuu wa mkoa , kwahiyo hali ikawa hivyo sikuwa na jinsi ya kujitetea .

Lakini niliamua kumdangaya tu , nikamwambia safari imeahirishwa bwana , mpaka tutakapowaambia hapo baadaye mwezi huu kwahiyo nitaenda mkoani singida au mtwara kwa kazi kama hizo “ Ohh yona unasema kweli ? nilivyokuwa nakungoja kwa hamu hivyo nikupe mambo ? na majambo ?”

Basi nilienda kidogo katika internet café kwa ajili ya kumwandikia email yule receptionist wa pale kumweleza hali halisi kisha nikampigia simu kumweleza kuhusu niliandisha katika email kwa kifupi alinielewa kwahiyo kazi ikawa kwake asiseme kama nimekuja mbeya na wala nikifika kule asiniite jina langu akinitaka aniite SHY tu mengine sijui .

Asubuhi yake ikafika yaani jumanne , niliamka katika saa 3 hivi asubuhi , hapo nilienda kuweka vitu vyangu katika hoteli moja eneo la meta mjini mbeya karibu na kituo changu cha kazi nikamuuliza tena yule receptionist kama yule dada anayeningoja yuko karibu au la , kweli yule dada alikuwa mbali kidogo .

Nikatoka hapo kuelekea katika kituo cha kazi kufanya ile iliyonipeleka pale , niliifanya kwa masaa 3 hivi ndio nilimaliza kwahiyo nikarudi zangu katika hoteli , huku nilienda tu kujisafi kwa mara ya pili kubadilisha nguo na kuvaa kama mtoto wa kijiweni halafu nianze kutembelea mitaa ya mji wa mbeya kuongea na watu haswa vijana .

Mbeya kuna mambo ya ajabu na wakati mwingine ya kutisha kama hujazoea , maajabu yake ni kwamba “ HUU NDIO MJI WA PILI KWA WINGI WA MAKANISA BARANI AFRIKA “ Ni mji wenye makanisa mengi kuliko yote Afrika Mashariki Na Kati ,huu wingi wa makanisa yaani ukitembelea hatua 30 unakuta kanisa mbele yako au kama sio kanisa unakuta sehemu ya mahubiri mbele yako hata pembeni yako .

Huu wingi wa makanisa sio hoja kwamba watu wa huku wameshiba neno la mungu kiasi kwamba wanaweza kubadili maisha yao na kuwa mazuri zaidi au kuwa bora zaidi la hasha , wamejawa na neno la mungu mpaka limepasuka yaani wamekinai neno la mungu sasa wanaona kuwa na makanisa ni fasheni .

Huu ndio mji unaoongoza kwa kukua kwa maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi katika afrika ukiachilia jberg , huu unafuatia , kutokana na kwanza uko Mpakani , watu wengi wa afrika ya kusini wanapoingia Tanzania kwa njia ya lami hupitia mbeya kuja dsm , wale wa Zambia nao ni mbeya , Botswana na kadhalika ni mji ulio katika majaribu mengi sana .

Unaona makanisa mengi , watu wengi wameokoka na kadhalika lakini watu wanaangamia kwa ugonjwa wa ukimwi kila kukicha na wenyewe wenyeji wa hapa wengi hawaamini kama kuna ukimwi wanaamini mtu akifariki basi amefariki kutokana na mungu kumwita amechoka maisha ya dunia , wengine ndio hizo imani zao akifa mwenzao amelogwa na mambo kama hayo .

Hapa mjini ukikutana na wasichana 5 basi 3 wanamarafiki wa kiume ambao sio wanafunzi wenzao yaani watu wa nje tu , wamachinga na madereva au watu wa shuguli zingine , hii inaadhiri sana hawa vijana utendaji wao madarasani , maishani na katika maamuzi mengine muhimu katika maisha yao kutokana na nguvu za watu wengine wa nje hawa wafanya biashara .

Mimi hoteli niliyofikia ilikuwa karibu na barabara kidogo , nilikutana na wanamuziki wa bendi ya Akudo Sound , hawa wanamuziki wacheza shoo wao wale wasichana wote ni chini ya miaka 22 , basi hapa katika hii hotel unachukuwa chumba halafu wahudumu wanakuuliza kama unapenda kupata dada wa kuishi nae wakati wote uko hapo katika hoteli .

Yaani huyu msichana atakuwa anakufulia nguo zako ulizokuja nazo na kukunyooshea wakati haupo , anakupa huduma ya ngono ( HII NDIO HUDUMA KUU ) , ukipenda atakuwa anakupikia pamoja na mambo mengine kukuogesha , na vitu kama hivyo , sasa unamwangalia huyu msichana mrembo ( WENGI WAO NI WAREMBO HASWA ) ametulia ana miaka chini ya 25 kwanini anakuja kujiuza huku , amekosa nii maishani mpaka amekuja katika hizi hoteli kujiuza .

Ukikataa kuchukuwa msichana inawezekana usiku wanakusumbua kwa kelele kule katika bar au dirishani mwako , wanakuuliza kama unataka huduma au la , kama hutaki wengine wanaaza kukutusi na maneno mengine ambayo siwezi kuyataja kama wewe shoga nini ? Unaliwa kiboga ? yote haya kisa umemkataa .

Ndio unaweza kuamua kumchukuwa , ukimchukuwa tu ujue sio wewe peke yako uliyemchukuwa labda wiki nzima hajalala kwao au kwake yuko pale anatoa huduma kwa wateja mbali mbali , kila siku yuko katika ngono na mambo mengine yasiyo na msingi kwa binadamu wa kawaida kama ameadhirika basi na wewe uko njiani , safari yako inakuja nap engine unaweza kuadhibiwa zaidi .

Saa zingine unaweza kutoka chumbani kwako katika corridor msichana anaweza kukuvulia chupi ? anakuonyesha alivyoumbika , ni kigiza hivi huoni vizuri lakini ukiona msiri wa chupi unalegea na kuteremka chini utasimama uangalie kunani , wengine utakuta wamesimama katika corridor na nguo zinazoonyesha maungo yao kazi ni kwako wewe mtazamaji yaani mimi niangalie nimekubali nichukuwe mzigo ?

Naweza kukubali , kukubali ni rahisi sana kwasababu inasemekana huyu msichana kukaa nae kwa usiku mmoja ni alfu 2 yaani hii alfu mbili hata kondom yaa maana hupati kama unaamua kulala nae na kutumia kinga , kinga zenyewe haziaminiki ya nini kufanya vile wakati najua wako zaidi yake ? na nikwambie siri wanawake wa mbeya wengi ni wanawake asili ya kiafrika yaani wamejazia ndio hapo sasa mate yanakutoka udenda njee , vishawishi na mambo mengine ya usheee .

Kwahiyo ndio hivyo , kesho yake nilitoka katika hoteli hii nikaenda katika hoteli ingine nikawe huru zaidi kwakuwa nilipenda kupiga picha mji ule wakati wa usiku niwatumie baadhi ya rafiki zangu wengine wanaopenda kujua zaidi kuhusu mji wa mbeya na mambo yake , ndio hivyo niliwakimbia hawa wadada mwaaah .

Siku ya pili ni kwenda kuandika report kuhusu ile kazi ya jana na kufanya majaribio kuhusu mashine zingine , kuwauliza maswali kadhaa kama wanamatatizo yoyote yale na kadhalika , kwahiyo hawakuwa na matatizo yoyote kwahiyo niliwaaga kutoka pale nikaanza safari ya kwenda tukuyu sikuwahi kufika tukuyu nilipenda kufika tu kwa kuwa kuna baadhi ya rafiki zangu wanatokea mkoa huu .

Nilifika pale muda wa saa 9 hivi jioni , nikatafuta sehemu ya kupumzika nikapata nikaenda kuhifadhi vitu vyangu , nikabeba kamera yangu , na kitabu changu kidogo kuanza kwenda mitaani , nilibahatika kuona internet café moja jirani pale , nikaingia ndani mule kufanya shuguli zangu .

Basi nilifika katika internet café hii niliwaambia watu kwamba niko mkoani mbeya sehemu inaitwa tukuyu , kuna baadhi ya watu ni wenyeji wa mkoa wa mbeya tulikuwa tunachat pamoja wengine wanatokea tukuyu na kyela , wakanielekeza makwao niwatembelee na wengine walihitaji salamu kutoka kwao .

Ndio hivyo nilipata marafiki wapya wa mkoani mbeya kw anjia ya mtandao , basi pale nilipokuwa jirani kidogo kama kilometa 10 hivi ndio sehemu ya kwanza nilitakiwa kwenda , nilifanikiwa kwenda mpaka kwa hiyo nyumba niliyoelekezwa na rafiki wa internet niliongea nao na kuwapa namba za simu za huyo ndugu yao aliye majuu , kwingine ni kyela lakini kyela mpaka kesho yake safari yangu ya mwisho .

Muda wa saa 3 hivi usiku nilitoka zangu kule mtaani nikarudi zangu katika nyumba niliyofikia , nilienda kuweka vitu vyangu na nikabadilisha mavazi kama ya kijana mtanashati , mwenye aibu sana , niliyekuwa mpweke nahitaji huduma Fulani ??? huduma ya ……?? Nikakaa pale katika bar , nikaagiza nyama choma nikawa nakula na glasi ya juisi .

Dada mmoja hivi ametokea zake huko sijui wapi akaja pale , akakaa mbele yangu nikamkaribisha vizuri sana kwa roho moja tukaanza kuongea , huyu msichana ni mrembo na amejazia kuanzia kigua , miguu na kadhalika hakika huyu ni masha alah kama nilivyokuambia wasichana wengi wa mkoa wa mbeya wamejazia au sio ?

Mrembo wa watu tukaongea kwa masaa 2 hivi mpaka saa 5 usiku , akaniomba namba ya simu nikampa , pia aliniuliza wapi ninapolala usiku huo , kama niko na mke au mtu maalumu usiku huo , nilimjibu sina niko mwenyewe tu na ninapenda kuwa mwenyewe hivyo hivyo inavutia zaidi au sio ?

Dada wa watu aliondoka , nami niliondoka zangu kurudi katika chumba kwa ajili ya mapumziko ya siku ile , basi nilipofika kule kwa hoteli muda kidogo yule dada aliniandikia sms inasema ‘ DEAR , UKO WAPI NIJE ? NINASIKIA BARIDI SANA NAHITAJI JOTO LAKO “ mhh nikakumbuka ni mambo yale yale nilivyokimbia kule mbeya mjini .

Nami nilimjibu “ JAMANI DEAR MBONA NA MIMI NASIKIA BARIDI NIMEJIFUNGIA CHUMBANI FUNGUO SIJUI IKO WAPI USIJE BWANA “ huyu dada akasoma msg yangu nilipokea jibu lake “ WE XXXNGE SANA , KWANINI ULINITONGOZA ? tukaendelea kubishana katika simu “ AHH NIMEKUTONGOZA ? SI BORA NIKATONGOZA NGOMBE AU MBUZI ? “

DADA : YAANI UNANIJIBU HIVYO ?
YONA : NDIO , BORA NITONGOZE NGOMBE

Basi nilizima ile simu yangu ili niwe huru zaidi nilale , kweli nikalala zangu mpaka usiku saa 10 hivi , nikaamka , nikaenda kwa yule mlinzi wa pale kumwambia anifungulie geti nataka kutoka nje akakataa akasema mpaka nimwambie receptionist wa pale naye alikuwa amelala , basi nilijaribu kumgongea hakuamka .

Uvumilivu ulinishinda , nilienda katika begi langu nikachukuwa vifaa nikatengua kitacha cha mlango wake mpaka ndani kwake nilimkuta yuko juu ya msichana Fulani katika fani ahaha , nilitaka kucheka lakini siku cheka , nilimfuata moja kwa moja mpaka pale nikamfunua shuka lile nikamshuka kitandani na kumpiga teke kidogo akajigonga katika kabati la nguo mule chumbani .

Nikimwomba sasa anifungulie mlango nitoke ndani ya ile hoteli kuna sehemu nataka kwenda , alitaka kuvaa nguo nikazichukuwa nguo pamoja na za yule msichana wote nikazitupa nje ya mlango ili anipe funguo nikafungue mwenyewe , alibisha nilivyomwomba basi nikamfuata tena kumtisha .

Ndio alisalimu amri akanipa funguo zile mimi huyo na begi langu nikatoka nje , nilikuta taxi pale karibu na hoteli lilinikimbiza mpaka kituo cha gari kupata basi la kuelekea kyela nikakata tiketi zangu pale na kupakiza vitu vyangu katika gari lile .

Kyela nilifika salama sana , nikafanya na kutekeleza yaliyonipeleka kule mwisho siku hiyo niliyo usiku nilirudi mbeya mjini ili nijiandae kwa safari ya kurudi zangu mjini dare s salaam kama kawaida , nilifika mbeya mjini katika saa 5 hivi za usiku moja kwa moja nilielekea katika nyumba ya wageni kwenda kupumzika .

Kesho yake ya asbuhi ilikuwa ni saa 11 hivi niliamka mapema nikajiandaa kwenda standi ya basi nikapata basin a safari ya kuja dare s salaam ilianza na kunoga kama kawaid nilifika jiji la mzizima nikiwa salama salmin na mwenye afya tele .

Nilifika muda wa saa 10 hivi , nikaja zangu hapa katika office kuleta report za huko kisha nikakimbilia katika mtando usiku huo huo kwa ajili ya kutuma hizi picha kwa watu Fulani marafiki zangu .

Na huo ndio ukawa mwisho wa safari yangu maridadi mkoani mbeya nilienjoy vya kutosha , karibuni nitaenda mkoani Mtwara , Lindi , Dodoma , Morogoro , Singida na Arusha kwa ajili ya kazi hizi hizi tuone itakuaje

Sikiliza tu

----+ I LOVE YOU EVE +----